Meneja Biashara CRDB Kyela Bwana Misape Tindwa akimkabidhi zawadi mmoja wa watoto wanaomiliki akaunti ya JUNIOR JUMBO waliohudhuria hafla ya MTOTO WA AFRIKA
Bwana Misape Tindwa akimkabidhi zawadi mtoto anayemiliki akaunti ya JUNIOR JUMBO katika hafla ya SIKU YA MTOTO AFRIKA
Wazazi na watoto wao wanaomiliki Akaunti za JUNIOR JUMBO wakiwa katika picha ya pamoja walipokuwa katika hafla ya kusherehekea siku ya MTOTO AFRIKA jana iliyofanyika CRDB BANK tawi la KyelaBenki ya CRDB wilayani Kyela imeungana na Afrika katika kusherehekea siku ya Mtoto wa Afrika jana tarehe 16 Juni 2015 .Benki hiyo imeshiriki siku hiyo kwa kuwaalika watoto wote wanaomiliki akaunti ya JUNIOR ACCOUNT wilayani humu katika Benki hiyo wilayani Kyela.
Akikabidhi zawadi kwa watoto waliohudhuria sherehe hiyo Meneja Biashara wa tawi hilo Bwana Misape Tindwa kwa niaba ya Meneja wa CRDB tawi la kyela ambazo ni fulana (tshirt) za bank hiyo na kalamu za wino (pen) amesema kuwa Benki hiyo inatambua umuhimu wa watoto na amewataka wazazi na walezi kuwapenda watoto.
Pia ameongeza kwa kueleza umuhimu wa wazazi kuwafungulia watoto wao Akaunti ya akiba kwa watoto ijulikanayo kama JUNIOR JUMBO ACCOUNT kwa faida ya maisha ya mtoto ya baadae.
Mmoja wa watoto walioshiriki katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za CRDB bank zilizopo sambamba na Barabara itokayo msikiti mkuu wa Kyela kuelekea Halmashauri ya Wilaya KyelaGeofrey Fungo ameishukuru bank hiyo kwa kutambua umuhimu wa maadhimisho ya mtoto wa afrika ambapo wilaya ya Kyela ni bank hiyo tu ilioadhimisha maadhimisho hayo.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni watoto wana haki ya kusikilizwa na kuhusishwa katika mambo mbali mbali ya muhimu.
Imeandaliwa na PUYOL B MWASAMPETA(0757337870)
KAMA UNA HABARI NA MATANGAZO WASILIANA PUYOL AU MOJA KWA MOJA
Post a Comment